WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA ZA UCHUMI WA BULUU PROF GURUMO.
Na Mwandishi wetu
Tanga
Wanawake nchini Tanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za Uchumi wa buluu kwani ni chanzo muhimu cha ajira na kuinua uchumi wa mtu mojamoja kwa jamii na Taifa kwa Ujumla, Katika Sekta hii ya Uchumi inaitaji kufanya kazi bidii na kuendelea kupata elimu na Uchukuzi
Hayo yamesemwa na Prof. Tumaini Gurumo , Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam kwenye siku ya Kimataifa ya wananwake katika Sekta ya Bahari yaliyoifanyika jijini Tanga.
Prof. Tumain akiwa anachokoza mada katika maadhimisho hayo amesema kuwa katika sekta ya maji kunafursa nyingi kwa wananwake wanaeza kufanya ili kuinua kipato, ili fursa hizo ziweze kupatikana zinaitaji kufanya kazi kwa bidii, kuendelea kujifunza teknolojia mpya zinazotokea kila siku, na kujiamini katika uchumi wa buluu. Kunafursa nyingi kwa wanawake katika uchumi wa buluu kama vile uhandisi,
Ubaharia,Usimamiaji wa Bandari na mambo mengine mengi pia kuhakikisha hata waliosemea masomo mengine wanaweza kama Sheria na Tehama wanaweza kujifunza kuhusu ubaharia’’ alisema Prof gurumo
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk Batilda Burian amesema kuwa maendeleo ya taifa hayawezi kupimwa kwa kiwango cha uwekezaji au ujenzi wa viwanda pekee, bali kwa namna serikali na jamii zinavyoweka fursa za usawa wa kijinsia katika ajira, hususan kwa watoto wa kike na wa kiume.
Namnukuu mwanafalsafa maarufu Plato, aliyewahi kusema kuwa "Kilimo cha jamii yoyote ni jinsi inavyowathamini wanawake", Dk Burian alisisitiza kuwa taifa linapaswa kujipangia malengo ya kuhakikisha usawa wa kijinsia unatekelezwa kikamilifu Tusiache mwanamke abaki ufukweni bali tunataka aingie ndani ya bahari," alisema kwa msisitizo..
Alieleza kuwa licha ya juhudi zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali, sekta ya bahari bado inatawaliwa na wanaume, huku takwimu zikionyesha kuwa wanawake wanaofanya kazi katika sekta hiyo ni asilimia 1.2 pekee.
Katika hatua ya kutia moyo, Dk Burian alipongeza Umoja wa Wanawake Wanaofanya Kazi katika Sekta ya Bahari katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) kwa kuanzisha programu ya 'Wakamate Wangali Wadogo' (Catch them Young) inayolenga kuelimisha na kuwahamasisha wanafunzi wa kike kujiunga na fani zinazohusiana na bahari.
Alisisitiza kuwa wanawake ndio uti wa mgongo wa sekta hiyo, akibainisha kuwa juhudi kama hizo zinaunga mkono maono ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ya kuwekeza kwenye elimu ya sayansi kwa watoto wa kike, ikiwemo kuanzishwa kwa shule maalum."
Hapa Tanga, kupitia uwekezaji wa Rais, tumeanzisha shule maalum ya watoto wa kike wilayani Kilindi ambayo imepewa jina la aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Beatrice Shelukindo," alisema.
Dk Burian pia alitoa wito kwa sekta binafsi inayohusika na bahari kuhakikisha usawa wa kijinsia unazingatiwa katika ajira.
"Kwa upande wake, Mwenyekiti wa WOMESA, Bi Fortunata Kikwaya, alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, kwa uwekezaji mkubwa walioufanya katika sekta ya bahari."
Sherehe hizi za nne zinaashiria maono yetu kuwa wanawake si wa kushirikishwa tu, bali ni wadau wakuu katika maendeleo ya sekta hii," alisema.
Bi Kikwaya alitaja mafanikio ya WOMESA kuwa ni pamoja na ongezeko la wanachama kutoka 24 mwaka 2021 hadi kufikia 174 mwaka huu, pamoja na kudhamini mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wanawake.
Kuhusu mpango wa 'Catch them Young', alisema tayari wametembelea shule 35 na kuanzisha vilabu tisa vya wanafunzi, vitatu kati yake vikiwa jijini Tanga.
Hata hivyo, alieleza kuwepo kwa mwamko mdogo wa wanawake kujiunga na WOMESA pamoja na uelewa mdogo kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya bahari.
Aliiomba Serikali kuanzisha utaratibu wa kutoa ufadhili wa masomo kwa watoto wa kike wanaotaka kusomea taaluma zinazohusiana na sekta ya bahari na kusaidia kuendeleza juhudi za kuwahamasisha kuingia katika sekta hiyo





0 Comments