WATAALAMU WA USAFIRISHAJI TANZANIA WAWEKA SHERIA MAHUSUSI YA USAFIRI.
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Wizara ya uchukuzi inaendelea na hatua ya kuweka Sheria mahususi ya usimamizi wa watalaamu wa usafirishaji nchini.
Akizungumza Jijini Dar es saalam Prof. Makame mbarawa mara baada ya mkutano wa chama cha watalaam wa Logistiki na Usafirishaji amesema kuwa kwa sasa wizara ya uchukuzi inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ikwemo mradi wa SGR.
“ Wizara yangu inaendelea na hatua za kuwezesha kutungwa kwa Sheria Mahsusi ya Usimamizi wa Wataalam wa Usafirishaji Tanzania (Transport Professionals Registration Board Act).hivyo Kupitia Sheria hiyo kutaanzishwa Bodi ya Usimamizi wa Wataalam wa Usafirishaji ambayo itakuwa na jukumu kubwa la kudhibiti maadili na utendaji kazi wa wataalam husika. “ Alisema Prof .Mbarawa.
Aidha Waziri Mbarawa ameongeza kuwa Serikali imejipanga vyema Katika kushirikiana na sekta binafsi ili kuweza kutekeleza miradi kwa utaratibu wa PPP katika ujenzi wa reli mpya ya kisasa (SGR) kutoka Mtwara - Mbambabay – Mchuchuma/Liganga (Km 1000) kwa ajili ya kuendelea kuifungua ushoroba wa Mtwara.
Kwa Upande wake rais wa chama cha wataalam wa lojistiki na usafirishaji Alphonce Mingira amesema kuwa chama hicho kinalengo la kusaidia watalaam na wafanyabiashara wa usafiri na usafirishaji Katika maendeleo ili kuona fursa zilizopo na kuweka mazingira Mazuri ya utendaji kazi kati Sekta Binafsi na Serikali.
Naye Mkurugenzi wa idara ya Udhibiti kiuchumi kutoka TCAA Daniel Malanga Amesema taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu kwa manufaa ya watanzania wote nchini.
Vilevile Mkutano huo umehudhuriwa na Taasisi zilizopo chini ya Sekta ya uchukuzi ambapo washiriki kutoka wizara ya Ujenzi, Tamisemi na vyuo vya elimu ya Juu.





0 Comments