Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya uvunjifu wa amani ya Oktoba 29, 2025 Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande amesema matukio ya ghasia za Oktoba 29, 2025 yalidhamiria kuzuia na kuvuruga uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
"Kutokana na ushahidi uliotolewa mbele ya Tume, lengo kuu la ghasia za Oktoba 2025 lilikuwa ni kuzuia na kuzuia uchaguzi Mkuu. Lengo hili linajidhihirisha kupitia vitendo mbalimbali ikiwemo kuharibu vituo vya kupiga kura, kushambulia askari kwenye vituo vya kupigia kura, mawakala na wasimamizi wa uchaguzi, kuharibu mali za wasimamizi wa uchaguzi, vitisho na madhara dhidi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura." Amesema Jaji Chande.Jaji Mstaafu Chande ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 23, 2026 mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar Es salaam, wakati akiwasilisha matokeo ya ripoti ya uchunguzi wa matukio ya wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2026.


0 Comments