🔷️🔷️MARIDHIANO YATAREJESHA UMOJA NA MSHIKAMANO WETU- BALILE

 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amesema ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuundwa kwa Tume ya maridhiano na Tume ya Upelelezi wa makosa ya Jinai yaliyotokea Wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kutaponya na kuwaleta tena Watanzania pamoja kama ilivyo tamanio la Watanzania wengi.

Balile ametoa kauli hiyo punde baada ya Rais Samia kupokea ripoti ya Tume huru aliyoiunda kuchunguza matukio ya Uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 leo Alhamisi Aprili 23, 2025 ambapo pia Rais Samia aliahidi kuunda Tume hizo ili kushughulikia mapendekezo yaliyotolewa leo na Tume ya Jaji Mohamed Othman Chande.


"Nchi ya Afrika Kusini iliunda tume ya maridhiano chini ya Askofu Desmond Tutu na kwakweli ilimaliza changamoto zao. Kubwa kuliko yote hapa tulipo tumeshafika, tuna wajibu wa kutoka na nimekuwa nikisema sisi kama Watanzania tukiharibu amani tutapigana na tukishapigana tutaitana kwenye meza ya mazungumzo kujadili namna ya kuleta amani, amani ambayo tulikuwa tumeishika mkononi, kwahiyo hatuna fursa nyingine zaidi ya hii kwamba imeshatokea, tufanye kazi kama Watanzania na waliohusika wawajibike binafsi." Ameongeza kusema Bw. Balile.

Post a Comment

0 Comments