NI WAJIBU KULINDA AMANI YA NCHI YETU, MWENYEKITI MCHANGE.


Na Mwandishi wetu,  Dar es alaam.


Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali za Taifa (MECIRA) Habibu Mchange amewataka watanzania wote nchini kuendelea kulinda Amani na utulivu katika kipindi hiki ambacho kumetokea na changamoto ya uharibifu wa mali Oktoba 29.

Akizungumza Na Wanahabari Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa kituo cha Wanahabari, watetezi wa rasilimali za taifa (MECIRA) Habibu mchange amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa kutoka vyama mbalimbali wanaendelea kuchochea uhalifu nchini hali ambayo inasababisha Athari za kijamii kutokea.


Kuna Viongozi kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wanaendelea kuchafua hali ya usalama nchini kwetu wakati kipindi cha uchaguzi mwezi Oktoba 29 walikataa kushiriki uchaguzi huo.


"Sisi kama watanzania hatuko tayari kuharibu amani ya nchi yetu kwa sababu ambazo hazina msingi kwani hupelekea majanga mbalimbali yakiwemo ukosefu wa huduma za Msingi" Amesema Mchange.


Aidha kila nchi ina kanuni na sheria ambazo zinahitaji kufwata hivyo suala la upotoshaji wa mambo yasiyofaa hayastahili kwenye nchi yetu.

Post a Comment

0 Comments