CHANIKA YAPAA KIMAENDELEO, MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

 

Na Mwandishi wetu,   Dar es Salaam


 Wananchi kata  ya Chanika wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa ya huduma za afya na elimu Wilayani humo, wakisisitiza umuhimu wa wazazi kuwaandikisha watoto wao katika msimu ujao wa masomo 2026, ili waweze kunufaika na uwekezaji mkubwa uliofanywa ndani ya Wilaya ya Temeke na Tanzania kwa ujumla.

Wananchi hao wameeleza namna ambavyo walilazimika kusafirisha miili ya wapendwa wao wanaofariki kwenda kuhifadhiwa Wilayani Kisarawe kutokana na kukosekana kwa Vyumba vya kuhifadhia maiti katika Kata yao ya Chanika kwenye Hospitali ya Nguvukazi.


Akizungumza na mwandishi wetu wa habari Bi. Jaliah Kabeya, Mkazi wa Chanika Jijini Dar Es Salaam amesema kwasasa katika sekta ya elimu na afya hakuna changamoto yoyote, akishukuru pia kwa ujenzi wa barabara za ndani ya Wilaya yao ikiwemo changamoto ya mafuriko Tazara suala ambalo lilikuwa likikwamisha shughuli za usafiri na usafirishaji ndani ya eneo hilo.


"Tunamshukuru Mungu na Mama Samia kwa hili, tumuombee dua ili aendeleze pale alipobakiza kwasababu yeye si malaika na hawezi kufanya yote kwa wakati mmoja na kwa haya aliyoyafanya pia ni muhimu kuwa na roho shukrani." Amesema Bi. Jaliah.


Mwananchi huyo pia ameshukuru kwa usimamizi wa mikopo ya Asilimia kumi ya Halmashauri inayotolewa kwa wanawake, Vijana na wenye ulemavu, akisema suala hilo limesaidia pakubwa kuwakwamua wananchi na umaskini, akisifu pia michakato yake na mikopo kuwa rahisi.

Post a Comment

0 Comments