Na Mwandishi wetu,Unguja
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya katika kuongeza jitihada za kuweza kuongeza ufanisi mkubwa katika saula zima la uwajibikaji na kujinza mambo mbali mbali imeamua kwenda kufanya ziara maalumu ya kikazi Zanibar katika visiwa vya eneo la Unguja ambayo itaweza kuwasaidia watendaji pamoja na madiwani katika kuongeza weledi na utekelezaji wa majukumu yao mbali mbali ya kila siku.
Yegella amesema kwamba lengo kubwa la Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwahudumia wananchi wake na kuleta chachu ya maendeleo na mabadiliko makubwa katika nyanja mbali mbali hivyo ana imani kwamba kufanyika kwa ziara hiyo kwa upande wa madiwani itawezamkuleta tija na mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kutokana na mafunzo ambayo watajifunza.
"Nashukuru sana mimi pamoja na baadhi ya waatendaji pamoja na madiwani wangu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya tumefika salama na tumepokelewa vizuri sana Zanzibar na kwamba tumekuja maalumu kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne ambapo tutakuwepo katika maeneo mabali mbali ya Unguja na wenyeji wetu akiwemo Mkurugenzi mtendaji wa mjini magharibi ametupokea kwa heshima zote,"amebainisha Bi. Yegella.
Kadhalika Mkurugenzi huyo amesema katika ziara hiyo wataweza kupata fursa ya kujifunza masuala mbali mbali na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza majukumu yao ikiwe pamoja na kutembelea miradi mbali mbali ya maendeeleo kwa ajili ya kujifunza jinsi wanavyoweka mikakati katika kutekeelza miradi hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya mjini Magharibi Bi. Sabra Machano amesema kwamba amefarijika sana na ujio wa ziara hiyo kutoka kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na kuahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali katika kipindi chote watakapokuwa katika ziara ya mafunzo hayo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya BI. Aiddah Haule amesema kwamba mafunzo ambayo watayapata wakiwa katika visiwa hivyo vya unguja yeye pamoja na jopo la madiwani pamoja na mkurugenzi wapo yatakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuleta mageuzi katika nyanja mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wananchi katika
maeneo yao mbali mbali.





0 Comments