Na Sheila Ahmadi , Ruangwa
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeanzisha kiwanda cha kuchakata chumvi katika eneo la Lingaula, Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi, kwa lengo la kuwawezesha wavunaji wa chumvi katika mikoa ya kusini kupata soko la uhakika na kuongeza thamani ya mazao yao.
Akizungumza kwenye maonyesho ya Madini Mkoani Lindi Wilaya ya Ruangwa Meneja wa Wachimbaji Wadogo wa Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) Mchagwa Chacha Marwa, amesema chumvi ni miongoni mwa madini yanayotambuliwa chini ya Sheria ya Madini, hivyo shirika hilo lina jukumu la kuwajengea uwezo wavunaji wa chumvi hususani katika mikoa ya kusini.kuanzishwa kwa kiwanda hicho kunalenga kutatua changamoto ya soko iliyokuwa ikiwakabili wavunaji wa chumvi, ambao hapo awali walilazimika kusafirisha mazao yao umbali mrefu kwenda Mkuranga na maeneo mengine ya Bagamoyo ambako kuna viwanda vya kuchakata chumvi.
wavunaji watapata fursa ya kufika kiwandani kujifunza teknolojia ya uchakataji wa chumvi na kupata huduma za kuchakata mazao yao, huku gharama za huduma hizo zikizingatiwa ili kupunguza gharama kwa mzalishaji na kuongeza kipato.
Kupitia kiwanda hicho kilichopo takribani kilomita tisa kutoka Nangurukuru kwa upande wa mtu anayesafiri kutoka Lindi, kina uwezo wa kuchakata kati ya tani tatu na tano za chumvi kwa saa.
mwitikio wa wananchi tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho umekuwa mkubwa, kutokana na kukiona kama suluhisho la changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa soko la chumvi katika mikoa ya kusini.
Vilevile STAMICO imelenga kununua chumvi kutoka kwa wazalishaji wadogo na wakubwa, ili kuwapa fursa ya kuuza mazao yao bila kulazimika kukodi magari kwa gharama kubwa na kusafirisha chumvi kwenda mikoa yenye viwanda vilivyo mbali.
Hata hivyo Tunacholenga ni kununua kutoka kwa mzalishaji mdogo ambaye hana uwezo wa kukodi gari kutoka Lindi, Mtwara au maeneo ya uzalishaji kwenda kwenye viwanda vingine. , tunanunua kutoka kwa wazalishaji wakubwa.
STAMICO imekuwa ikipokea simu nyingi kutoka kwa wavunaji na wafanyabiashara wanaotaka kufahamu namna ya kuuza chumvi zao pamoja na huduma zinazotolewa na kiwanda hicho.
Aidha Kufikia sasa kiwanda kimenunua takribani tani 250 za chumvi kutoka kwa wazalishaji, huku maandalizi yakiendelea kwa ajili ya kuanza uzalishaji mkubwa.
Sanjari na hayo STAMICO imeanza maandalizi ya kufungasha na kuweka chapa ya bidhaa hiyo ili iweze kusambazwa katika masoko mbalimbali nchini.
Nitoe Wito kwa wafanyabiashara wa chumvi kufika katika ofisi za STAMICO kwa ajili ya kupata uwakala wa kusambaza bidhaa hiyo.
Katika Hatua nyingine STAMICO inalenga kuwashirikisha wananchi katika biashara ya chumvi, ikiwemo kuwawezesha kupata mawakala na kushiriki katika usambazaji wa chumvi itakayozalishwa na kiwanda hicho.


0 Comments