πŸ›‘πŸ›‘πŸ›‘GGM YATOA MCHANGO KUIMARISHA HAKI ZA WAFANYAKAZI WAZIRI SANGU

 

Na Sheila Ahmadi, Geita


wawekezaji katika sekta ya madini wamepongezwa kwa kushiriki katika kuimarisha hifadhi ya jamii na kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao, ikiwemo usalama na afya mahali pa kazi.

Akizungumza Mkoani Geita  kwenye Maonyesho ya madini Mara baada ya  kutembelea banda la Geita  Gold  Mine (GGM) Waziri  Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira ,na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amesema kuwa  waajiri katika sekta ya madini, ikiwemo Geita Gold Mine  (GGM), wamekuwa wadau muhimu katika mnyororo mzima wa hifadhi ya jamii, kutokana na ajira wanazozalisha kwa Watanzania.


 waajiri wanapaswa kuhakikisha wanazingatia sheria na viwango vya kazi, kulinda usalama na afya za wafanyakazi, pamoja na kuhakikisha michango yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii inawasilishwa kwa wakati.


Vilevile  GGM imetoa ajira nyingi kwa Watanzania, hivyo waajiri wanapaswa kuzingatia sheria za kazi, usalama na afya mahali pa kazi, pamoja na kuhakikisha michango ya wafanyakazi inapelekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii,” amesema.


Nitoe  pongezi  kwa  GGM  kwenda hatua zaidi ya kutekeleza wajibu wake wa kawaida kama mwajiri, kwa kushiriki katika shughuli zinazolenga kulinda na kutetea haki za wafanyakazi.


Aidha ni jambo la nadra kwa mwajiri kushiriki moja kwa moja katika jitihada za kuimarisha mifumo inayolenga kutatua migogoro ya kikazi na kulinda haki za wafanyakazi.


Hata hivyo  GGM imeunga mkono ujenzi wa ofisi za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), hatua ambayo imeelezwa kuwa itasaidia kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma kwa wafanyakazi na waajiri.


Katika hatua nyingine  Waziri Sangu ameongeza kuwa  ujenzi wa ofisi hizo umefikia hatua za mwisho, jambo litakalowezesha huduma za usuluhishi na utatuzi wa migogoro ya kikazi kupatikana kwa urahisi zaidi.


“Ni nadra sana kuona mwajiri akishiriki katika jambo la utetezi wa wafanyakazi na kutoa ufadhili wa kujenga ofisi za CMA. Kwa taarifa nilizonazo, ofisi hii ipo katika hatua za mwisho,” amesema Waziri Sangu".


Aidha, amempongeza Mbunge wa Mkoani humo Mhandisi Chacha Mwita wambura pamoja na wadau wengine walioshiriki katika kuanzisha na kuendeleza mpango huo, akieleza kuwa mchango wao unaonyesha dhamira ya kuimarisha sekta ya madini na ustawi wa wafanyakazi.


 ushiriki huo unaonyesha kuwa uwekezaji katika sekta ya madini haupaswi kuishia katika uzalishaji na mapato pekee, bali pia unapaswa kugusa maisha ya wafanyakazi na jamii inayozunguka maeneo ya migodi.

Post a Comment

0 Comments