Na Mwandishi wetu, Tanga
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi na ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Tanga kutafungua fursa mpya za kiuchumi, kuongeza uwekezaji na kuboresha huduma za usafiri wa anga katika Mkoa wa Tanga na maeneo ya jirani.
Kihenzile amesema hayo wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, ambapo alieleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa, huku akisisitiza kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga kwa manufaa ya wananchi.Amesema kukamilika kwa uwanja huo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo, kuimarisha shughuli za biashara na utalii, pamoja na kuongeza mchango wa sekta ya usafiri katika kukuza uchumi wa Taifa.
Aidha, Kihenzile amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuongeza kasi ya kazi ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati uliopangwa, huku akizingatia viwango vyote vya ubora vilivyoainishwa katika mkataba"Amesema Kihenzile


0 Comments